Katika hafla ya pongezi za viongozi China na Urusi kwa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Urusi, rais wa China amemwambia mwenzake wa Urusi leo Jumatano Oktoba 2 kwamba yuko tayari “kuendeleza” ushirikiano kati ya Moscow na Beijing, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.
Xi Jinping amesisitiza kwamba China iko “tayari kuungana na Bw. Putin katika kuendeleza daima ushirikiano wa kisayansi wa kimataifa kati ya nchi (zetu) mbili,” linabainisha shirika la habari la Xinhua.
China inajionyesha kuwa haina upande wowote katika mzozo wa Ukraine na inahakikisha kwamba haitoi silaha yoyote kwa upande wowote. Lakini Marekani na nchi za Ulaya mara kwa mara wanaishutumu kwa kuipa silaha Urusi, inayolengwa na vikwazo muhimu vya nchi za Magharibi, msaada muhimu wa kiuchumi kwa juhudi zake za vita.
Mnamo mwaka 2023, biashara kati ya China na Urusi ilifikia kiwango cha rekodi.
Moscow na Beijing wanasema wanapinga “utawala wa Magharibi,” hasa kile wanachoona kama Marekani kutaka kutawala dunia.
Kiongozi huyo wa China anatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kilele wa BRICS huko Kazan, magharibi mwa Urusi, mwezi Oktoba, ambapo anatazamiwa kukutana na rais wa Urusi. Ikiwa na wanachama wanne (Brazil, China, India na Urusi) ilipoundwa mwaka wa 2009, kambi ya BRICS, Afrika Kusini ilijiunga na muungano huo mwaka 2010 na kupanuliwa mwaka huu hadi nchi nyingine kadhaa zinazoinukia, zikiwemo Misri na Iran.