AyoTV

VIDEO: Siku 15 baada ya operation ya kuondoa wavamizi wa hifadhi Kagera

on

Kufuatia operation iliyoanza march 30 mwaka huu mkoani Kagera kwa ajili ya kuondoa mifugo na wananchi wavamizi waliokuwa wakiendesha shughuli za kibinadamu katika mapori ya akiba,mistu ya hifadhi pamoja na mapori tengefu,imetolewa hatua iliyofikiwa mpaka siku ya jana.

Akitoa taarifa hiyo mkuu wa mkoa Kagera meja Jeneral mstaafu Salum Kijuu amesema kuwa wamefanikiwa kukamata mifugo 5,939,watuhumiwa 185 wamekamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria ambapo wamefunguliwa mashitaka,kesi zinaendelea kusikilizwa na wengine tayari wamehukumiwa.

Aidha amesema kuwa serikali inasubili utaratibu wa kisheria mahakamani kukamilika kwa mifugo iliyotaifishwa na ile itakayoendelea kutaifishwa ili mifugo hiyo iweze kuuzwa kwa mnada wazi na kuruhusu kila mwananchi kushiriki mnada huo.

? LIVE: JPM kwenye uzinduzi wa Hostel UDSM 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments