Katika kuunga mkono dira President Magufuli ya Tanzania ya viwanda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameziagiza Manisapaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam kubadilisha mfumo wa utoaji 10% kwa kina mama na vijana ili fedha hizo ziweze kuleta tija katika utekelezaji wa Tanzania ya viwanda.
RC Makonda amesema mfumo wa sasa hauna utambuzi wa kutosha kwa vijana na kina mama kutokana na makundi hayo kutawanyika kibiashara jambo linalosababisha changamoto ya ufuatiliaji wa mikopo hiyo, na badala yake kuzitaka Manisapaa kutenga maeneo maalum ya uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya makundi hayo, hatua itakayowaweka pamoja na kutoa fursa kwa Serikali ya Mkoa kuwahudumia vizuri.
Aidha, katika kutekeleza mpango huo RC Makonda leo ameamua kuzindua majengo yatakayotumika kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo katika eneo la Mwananyamala Manisapaa ya Kinondoni ili kuzihimiza Manisapaa nyingine kuiga mfumo huo.
RC Makonda kasitisha bomoabomoa ya zaidi ya nyumba 17,000
“Hakuna atakayewabomolea nyumba zenu” – RC Makonda