Top Stories

Meya Ubungo baada ya uzinduzi wa vitambulisho matibabu bure kwa Wazee

on

Manispaa ya Ubungo leo September 4, 2017 imezindua vitambulisho vya huduma za afya bure kwa wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea ambapo wazee 7,299 kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bure katika awamu ya kwanza.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amesema anafurahia tukio hilo la kihihistoria ambalo litahakikisha wazee wanapatiwa matibabu bure akitoa shukrani kwa Serikali kuonesha nia na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Halmashauri mbalimbali kuboresha afya za wazee.

>>>”Huduma hii tumeweka katika namna ambayo hatujatoa zabuni kwa mtu wan je. Tumenunua vifaa vyetu kama Manispaa ya Ubungo visivyozidi Milioni 100 na tutavitumia kugawa kadi kwa wazee wote.

“Lengo ni kufikia wazee wote 61,000. Leo huduma yetu imezindua awamu ya kwanza tumetoa vitambulisho 7,299.” – Meya Jacob.

UZINDUZI! Ni ule mpango wa huduma ya afya bure kwa Wazee

WAZIRI UMMY! “Hatukatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya Dawa lakini…”

Soma na hizi

Tupia Comments