Top Stories

TUJIKUMBUSHE! Vitu vya kukumbukwa kila September 11 Marekani

on

Leo September 11, 2017 ni kumbukumbu ya miaka 16 tangu kufanyika kwa shambulizi la kigaidi Marekani September 11, 2001 ambapo nchi hiyo inaikumbuka sana siku hiyo hasa kutokana na kugharimu maisha ya watu takriban 3,000 na kujeruhi vibaya watu 6,000 huku ikiisababishia nchi hiyo hasara ya Dola Bilioni 10 ambazo ni zaidi ya Tsh Trilioni 22.

Siku hii hujulikana kama September 11 ambapo magaidi 19 wa Kundi la Al-Qaeda wakiongozwa na mshukiwa namba moja Osama bin Laden waligawanyika katika ndege nne ambapo katikati ya safari waliziteka ndege hizo kwa lengo la kufanya shambulizi.

Ndege mbili kati ya hizo zilielekezwa na kugonga majengo mawili marefu yanayotazamana yaliyoitwa ‘Twin towers’ katika kituo cha Biashara cha Dunia ‘World Trade Center ama WTC’ katika mji wa New York ambapo muda mfupi baada ya mlipuko yaliporomoka.

Ndege ya tatu ilielekezwa katika Makao Makuu ya Idara ya Ulinzi Pentagon lakini ndege ya nne haikufanikiwa kufika sehemu iliyolengwa na badala yake ilikwenda kulipuka katika mji wa Pennsylvania.

ULIPITWA? TAMKO LA CHADEMA KUHUSU KUSHAMBULIWA KWA RISASI TUNDU LISSU

Soma na hizi

Tupia Comments