Top Stories

KENYA: Mwanafunzi wa Kidato cha Nne kakamatwa na silaha shuleni

on

MWANAFUNZI wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Orero iliyopo Homa Bay, Kenya amekamatwa Jumanne baada ya kukutwa bastola.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17 anadaiwa kuionesha silaha hiyo kwa wanafunzi wenzake ambao baadaye walimripoti kwa uongozi wa shule na kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyowasilishwa Mahakamani, Polisi wanapanga kumshtaki kwa kumiliki pistol HK45, yenye namba 25094705 kinyume na kifungu cha 34(1) cha Sheria ya Silaha za moto.

Mwanafunzi huyo aliwaambia wapelelezi kuwa aliipata silaha hiyo kutoka kwa ndugu yake aliyekuwa anaishi Marekani ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Jaramogi Oginga Odinga University ingawa ripoti zilizowasilishwa Mahakamani zimedai aliichukua silaha hiyo chumbani kwa ndugu yake huyo katika Kaunti ya Siaya.

BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Yusuf Manji

 

Soma na hizi

Tupia Comments