Top Stories

HALIMA MDEE MAHAKAMANI! Upelelezi kesi yake umekamilika, kilichoamuliwa je?

on

Upelelezi wa kesi ya kumtolea lugha chafu Rais John Magufuli inayomkabili, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi leo September 12, 2017 amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika ambapo ameiomba Mahakama hiyo ipange tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali (PH).

Baada ya kusema hayo, Wakili wa Mdee, Peter Kibatala alidai kuwa wanaondoa mapingamizi yao ya kwamba Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi October 11, 2017 kwa ajili ya (PH).

ULIPITWA? DC Ally Hapi alivyoagiza kukamatwa kwa Mbunge Halima Mdee

Soma na hizi

Tupia Comments