Top Stories

HII KALI! Wamesafiri kutoka India hadi Marekani kumpiga mkwe wao

on

Wanandoa wawili wenye asili ya India Jasbir mwenye mika 67 na mkewe Bhupinder Kalsi mwenye miaka 61 pamoja na mtoto wao wa kiume Devbir Kalsi mwenye umri wa miaka 33, wanashikiliwa na Polisi Marekani baada ya wanandoa hao kusafiri kutoka India hadi Florida, Marekani kwa lengo la kumpiga mke wa mtoto wao huyo kwa sababu si mtiifu kwao.

Mwanamke huyo anayeitwa Silky Gaind, 33, alipiga simu kwa wazazi wake walioko India na Polisi kuwajulisha kuwa amefungiwa ndani na anapigwa na mumewe na wakwe zake ndipo Polisi walipofika eneo hilo kumwokoa ambapo alikuwa anapigwa akiwa na mtoto wake.

Kwa mujibu wa Polisi walipofika eneo hilo walikuta mlango umefungwa na kuamua kuuvunja na walipoingia ndani waliwakuta watatu hao wakimshambulia mwanamke huyo huku taarifa zikieleza kuwa ni tabia ya mwanamme huyo kumpiga mkewe na wakati huu akaamua kuomba msaada wa wazazi wake.

ULIPITWA? WAZIRI UMMY! “Hatukatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya Dawa lakini…”

Hii je? HALI YA HEWA: Ya kufahamu kuhusu mwelekeo wa mvua za vuli

 

Soma na hizi

Tupia Comments