Top Stories

UPDATES: Mbowe kaeleza kwa nini Tundu Lissu kapelekwa Nairobi kutibiwa

on

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Freeman Mbowe leo September 10, 2017 amebainisha kuhusu sababu kuu zilizofanya kuchukua uamuzi wa kumpeleka Nairobi, Kenya Mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu na dereva wake, Adam Simon baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Alhamisi ya September 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Dodoma.

Mwenyekiti Mbowe amesema walilazimika kumsafirisha Tundu Lissu kwenda Nairobi, Kenya kwa sababu tatu kubwa ambazo ni;

  1. Maisha ya Mhe Lissu yalikuwa hatarini sana na palihitajika matibabu maalum na ya haraka sana kutoka kwa Madaktari Bingwa wa kutosha sambamba na vifaa tiba visivyo na shaka yeyote ili kuokoa maisha yake kufuatia kazi kubwa na ya kupongezwa ya awali iliyofanywa na Madaktari wetu kadhaa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
  2. Hofu Kuu ya usalama wa Mhe. Lissu na dereva wake ilitanda kote nchini Tanzania baada ya shambulio dhidi ya Uhai wao kushindwa kufanikiwa. Busara ya ki-usalama ilitulazimisha kuwatoa wahanga nje ya mipaka ya nchi hadi hapo usalama wao utakapohakikishwa.
  3. Upande wa Uongozi wa Bunge na Serikali ulisisitiza kuwa Mhe. Lissu apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kama sivyo hawatakuwa tayari kubeba gharama yeyote inayohusiana na matibabu yake. Upande wangu na Wabunge wetu wa UKAWA ulisisitiza Mhe. Lissu apelekwe moja kwa moja Nairobi na kama Bunge na Serikali hawatakuwa tayari kubeba gharama za kuokoa maisha ya Mhe. Lissu, basi sisi na Watanzania wenye mapenzi mema watachangia gharama hizo za kuokoa maisha kitibabu na kiusalama.

Aidha, akizungumzia hali ya Lissu tangu alipofikishwa Nairobi kwa ajili ya matababu, Mwenyekiti Mbowe alisema baada ya kufika Nairobi kwa ndege maalum ya kukodi walipokelewa na madaktari Bingwa kutoka Hospitali Kuu ya Nairobi na kukimbizwa moja kwa moja hospitali ambapo kazi kubwa ya kuendelea kuokoa maisha yake ilifanywa usiku kucha na jopo la madaktari wa fani kadhaa wasiopungua kumi.

Mbowe amesema kuwa tangu Lissu amefikishwa Nairobi, amekuwa akipatiwa matibabu saa zote mfululizo yakihusisha upasuaji kadhaa na uangalizi muhimu katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU).

Kutokana na kupatiwa matibabu na madaktari, kwa mara ya kwanza, Lissu jana jioni aliongea na mkewe Alucia kisha baadaye alizungumza na Mbowe, akisema “Mwenyekiti, I survived to tell the tale….Please keep up the fight” na leo Jumapili amerudishwa chumba cha upasuaji kuendelea na upasuaji mwingine.

”Lissu hakupigwa risasi 30, ni uongo” – Kubenea

Soma na hizi

Tupia Comments