AyoTV

EXCLUSIVE: Ilipofikia video ya Joh Makini na Davido

on

Staa wa Hip Hop kutoka kundi la WEUSI ambaye anatamba na wimbo wake wa ‘Waya’ Joh Makini ameelezea kinachoendelea kuhusu ujio wa video ya wimbo wake ambao amemshirikisha staa wa Nigeria, Davido.

Kwenye exclusive interview na Ayo TV na millardayo.com Joh Makini amesema kuwa ameshakabidhiwa video hiyo na Director lakini anazipa kwanza nafasi nyimbo za YA KULEVYA na WAYA ziendelee kupata airtime akiamini kuwa zinafanya vizuri halafu baadaye ataiachia video mpya.

Mbali na ujio wa video hiyo mpya, Joh Makini amegusia taratibu za kutengeneza video ya wimbo wa Ya Kulevya akisema kuwa watatengenezea papa hapa Tanzania ambapo itaongozwa na Mtanzania huku akisema kundi hilo litaendelea kufanya show pamoja na uwepo wa funga mwaka na WEUSI baadaye mwaka huu.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza…

VIDEO: Alichokifanya Joh Makini Club 71, Tegeta usiku wa kuamkia May 1

Soma na hizi

Tupia Comments