Top Stories

Taasisi zaidi ya 30 zilizosainishwa na Hazina kuboresha huduma

on

Ofisi ya Msajili wa Hazina leo imesainisha mikataba ya utendaji wa fedha na taasisi na mashirika mbalimbali ya Umma zaidi ya 30 katika sekta za afya elimu, ustawi wa jamii na nyinginezo ikiwa ni moja ya njia ya kuboresha huduma nchini.

Msajili wa Hazina Osward Mashindano amesema mikataba inalenga kushauri Serikali, kufuatilia pamoja na kusimamia mashirika ya Umma katika utendaji wake na kufanya tathmini ya utekelezaji wa yaliyokubaliwa katika mikataba hiyo na kwa kiasi gani malengo yamefikiwa.

>>>”Kuna Taasisi 265 ambazo ni muhimu katika kuchangia pato la Taifa na katika uzalishaji mali, ongezeko la fursa za ajira na mengineyo ambayo yanasaidia katika kukuza uchumi wa nchi.” – Osward Mashindano.

ULIPITWA? Mpango wa huduma ya afya bure kwa Wazee uliozinduliwa na Waziri wa Afya

LISSU MAHAKAMANI TENA: Ni kwenye kesi ya ‘Dikteta Uchwara’ inayomkabili

Soma na hizi

Tupia Comments