Top Stories

Flaviana Matata akabidhi madarasa na ofisi ya Mkuu wa Shule alivyovijenga

on

Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata amekabidhi jengo la madarasa mawili yatakayotumika na darasa la sita na la saba pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule katika Shule ya Msingi Msinune iliyopo wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Flaviana ameeleza kuwa lengo kuu la kujenga jengo hilo ni kusaidia jitihada za kuinua elimu nchini kwa kuboresha miundombinu ya kusomea.

Mwanamitindo huyu alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na wanakijiji wa kijiji hicho cha Msinune mwaka 2014 ambao walimpatia jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja na kumalizia ujenzi wa madarasa.

“Sisi kama vijana wa Tanzania tunalo jukumu la kujitokeza na kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine muhimu nchini kwa kuwa hili sio jukumu la serikali peke yake.” – Flaviana Matata

“January nimesurrender ” Aunt Ezekiel kafunguka Ugumu wa January

Alichoongea Jokate kwenye mazishi ya mama mzazi wa Johari

Soma na hizi

Tupia Comments