Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kutoa uamuzi mdogo wa zuio la muda la kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Viti Maalum wa Chama cha Wananchi CUF walioteuliwa na Chama hicho ili kuziba nafasi za Wabunge 8 waliofutwa uanachama August 17, 2017.
Hatua hiyo inatokana Wabunge 8 na Madiwani 2 waliovuliwa Uanachama na Prof. Lipumba kufungua kesi nyingine Mahakamani hapo wakipinga kuvuliwa uanachama na kutaka kuziuia kuapishwa kwa Wabunge wapya.
Maombi ya Wabunge na Madiwani hao yalitarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji Lugano Mwandambo, lakini Mawakili wa Serikali wakiongozwa na Vincent Tango waliwasilisha pingamizi la awali wakiomba Mahakama isiyasikilize.
Kutokana na hatua hiyo, leo Jaji Mwandambo, anatarajia kutoa uamuzi mdogo wa kuzuia ama kutozuiwa kuapishwa kwa Wabunge hao wakati kesi ya msingi ikisubiri kusikilizwa.
Akizungumza nje ya Mahakama, Wakili wa Wabunge na Madiwani hao waliofukuzwa, Peter Kibatala amedai kuwa wameiomba Mahakama iamuru hali ndani ya Chama iendelee kuwa kama ilivyo sasa hadi siku ya uamuzi wa pingamizi hilo.
Kibatala amedai kuwa kifungu cha sheria kilichopingwa awali na kusababisha maombi yao kutupwa, wamekibadilisha na kuja na kifungu cha 95 CPC.
PROF. LIPUMBA TENA: Ni kuhusu Wabunge wapya walioteuliwa…tazama kwenye hii video!!!!