Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: UVCCM wamewajibu BAVICHA kuhusu ishu ya Lissu kupigwa risasi
Share
Notification Show More
Latest News
Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
June 2, 2023
Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest
June 2, 2023
Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano
June 2, 2023
Amnesty yaonya Iran dhidi ya Kunyonga kwa Kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya
June 2, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > UVCCM wamewajibu BAVICHA kuhusu ishu ya Lissu kupigwa risasi
Top Stories

UVCCM wamewajibu BAVICHA kuhusu ishu ya Lissu kupigwa risasi

September 10, 2017
Share
2 Min Read
SHARE

Umoja wa Vijana wa CCM ‘UVCCM’ umelitaka Baraza la Vijana wa CHADEMA ‘BAVICHA’ kuacha kiherehere cha kuingilia taratibu za kiutawala na upelelezi yanapotokea masuala mazito, ikiwemo tukio la kushambuliwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na matukio ya watu kutekwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM (MNEC), Shaka Hamdu Shaka amesema September 9, 2017 aliwasikia BAVICHA kupitia kwa Katibu Mkuu wake wakitoa maneno ya kebehi yanayojenga utata na mkanganyiko akidai yanapalilia chuki na uhasama.

>>>”Matamshi ya BAVICHA yana nia na lengo la kupalilia chuki na hasama kwani yamethubutu kuingilia medani za ki-intelejensia na upelelezi kufuatia tukio la kusikitisha la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na watu wasiojulikana.”

Aidha, amesema kuwa sehemu kubwa katika maelezo ya viongozi wa BAVICHA haikuonyesha ukomavu wala hekima ukilinganisha na ukubwa wa tatizo la kushambuliwa kwa Lissu.

>>>”Tukio la kushambuliwa kwa Lissu si jambo dogo na jepesi kama inavyochukuliwa na BAVICHA, kwani kitendo cha Mwenyekiti na Katibu wake kuishutumu Serikali ni ukosefu wa adabu.”

Shaka amesema yapo matukio mengi ya ujambazi yamewahi kutokea na kupoteza maisha ya watu wakiwemo viongozi wa juu kabla ya tukio la Lissu akilitaja tukio la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Aaman Karume ambaye alipigwa risasi nane kifuani.

>>>”UVCCM kwa mara ya kwanza tunaunga mkono matamshi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliposema huu si wakati wa kunyoosha vidole vya lawama na shutuma huku akivitaka vyombo vya usalama vitimize wajibu wao kiufundi.”

BREAKING: TAMKO LA BAVICHA BAADA YA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

Watu 30 na Magari wakamatwa Dodoma, Dereva wa Lissu aitwa

TAMKO LA CHADEMA KUHUSU KUSHAMBULIWA KWA RISASI TUNDU LISSU

You Might Also Like

Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi

Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest

Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano

Amnesty yaonya Iran dhidi ya Kunyonga kwa Kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya

TAGGED: CCM, TZA HABARI
Millard Ayo September 10, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Alikiba kaimba Seduce me mara 3 Arusha
Next Article President Magufuli kafanya uteuzi wa Jaji Mkuu leo September 10, 2017
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
Top Stories June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
Top Stories June 2, 2023
Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest
Sports June 2, 2023
Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano
Top Stories June 2, 2023

You Might also Like

Top Stories

Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi

June 2, 2023
Top Stories

Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

June 2, 2023
Sports

Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest

June 2, 2023
Top Stories

Amnesty yaonya Iran dhidi ya Kunyonga kwa Kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya

June 2, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?