Kesi inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent, Innocent Mushi na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Longino Nkana leo September 28, 2017 imeshindwa kusikilizwa baada ya Hakimu kuutaka upande wa mashtaka kurekebisha hati ya mashtaka.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa upande wa utetezi, Method Kimomogolo kuweka pingamizi katika kosa namba moja na namba tatu kwa mshatakiwa wa kwanza ambaye ni mmiliki wa Shule hiyo Innocent Moshi anayetuhumiwa kwa makosa manne huku Makamu Mkuu wa Shule akituhumiwa kwa kosa moja
Makosa hayo ni kuruhusu gari kubeba wanafunzi bila kuwa na kibali, kuruhusi gari kutembea barabarani bila kuwa na bima, kushindwa kuwa na mkataba wa kazi na dereva, kuzidisha abiria 13 kwenye gari lililokuwa limebeba wanafunzi.
Aidha, kosa linalomkabili Makamu Mkuu wa Shule hiyo Longino Mkana ni kuruhusu gari hilo kuzidisha abiria 13.
Hakimu Desdery Kamugisha ametolea uamuzi mapingamizi mawili yaliyotolewa na upande wa Utetezi kuhusu kupinga kosa namba moja na namba tatu na kuwataka kubadilisha hati ya mashataka kutokana na kuwepo kwa mapungufu katika hati hiyo.
Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi October 6, 2017.
Manusura wa ajali ya basi la Shule ya Lucky Vincent walivyowasili