Leo October 4, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi katika kesi ya uchochezi ‘Dikteta Uchwara’ inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kama ana kesi ya kujibu ama la kwa sababu anaumwa.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Inspekta Said Hamis amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya uamuzi mdogo lakini mshtakiwa (Lissu) anaumwa na amelazwa Chandaria Accident and Emergency Nairobi Hospital, Kenya.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi November 16, 2017.
Katika kesi hiyo, Tundu Lissu anadaiwa July 28, 2016, katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa:
“Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidiktekta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote. Huyu Diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.”’
BREAKING: Mbowe asema alipo Dereva wa Lissu na kwanini hakuripoti Polisi
BREAKING NEWS: Freeman Mbowe karudi Dar, kaongea yote ya Tundu Lissu kwa mara ya kwanza toka alipopigwa risasi