Jumatano September 27, 2017, Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi ya utakatishaji fedha na kughushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ bado lipo kwa DPP.
Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini jalada la kesi bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Aidha, amedai kuwa DPP ataangalia kama ameridhishwa na kesi hiyo ama ala, ambapo watasubiri kama uchunguzi umekamilika.
Baada ya kuelezwa hayo, Wakili wa utetezi, Evidius Mtawala kwa sababu ya taratibu zinazoendelea ni za kiofisi wanatumai jalada litaharakishwa.
Kutokana na hatua hiyo Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi October 4, 2017.
Evans Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha Dola za kimarekani 300,000.
WATU WASIOJULIKANA: “Dakika zao zinahesabika” – Mwigulu