Ad

Top Stories

Pesa ilizokusanya Polisi DSM ndani ya siku Tano kwa makosa ya Barabarani

on

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani imefanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 475.3 kutokana na tozo za makosa mbalimbali ya Usalama Barabari katika kipindi cha siku Tano kuanzia September 6 hadi 11, 2017.

Kiasi hicho cha fedha kinatokana na kukamata magari 13,220, Pikipiki 656, Daladala 7,930, Magari mengine (ya binafsi na malori) 5,290 na Bodaboda waliofikishwa Mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmet na kupakia mishkaki 55 ambapo hufanya jumla 15,940.

Kamanda Mambosasa kazungumza na Wanahabari na kuelezea mwenendo wa hali ya usalama Dar es Salaam…tazama hapa kwenye hii video

 

Soma na hizi

Tupia Comments