Breaking News

BREAKING: Zitto Kabwe kafikishwa Dodoma, amewekwa Central Police

on

Jioni ya jana September 20, 2017 kulikuwa na taarifa kwamba Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye ni kiongozi wa Chama cha ACT WAZALENDO Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi.

Sasa leo September 21, 2017 taarifa kutoka Chama hicho zinasema kuwa Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe ameshafikishwa Dodoma akiwa chini ya uangalizi wa Polisi na sasa yupo Central Police Dodoma.
Aidha, taarifa hizo zimesema kuwa, Zitto anatarajia kwenda kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge muda mfupi ujao.

Endelea kukaa karibu na millardayo.com na APP mpya ya ‘millardayo‘ kwa wenye simu za ANDROID ili kupata kila kitachonifikia.

ULIPITWA? Zitto Kabwe akamatwa na Polisi Airport

Soma na hizi

Tupia Comments