Habari za Mastaa

Kwenye stori kubwa >> Roberto na collabo TZ? album ya Weusi? Kala Jeremiah na ngoma mpya.. (+Audio)

on

Muziki umebadilika siku hizi, watu wanauza shows na maisha yanaenda sio kama zamani ile ishu ya kuuza album, Weusi wana mawazo tofauti kuhusu wazo hilo… Nick wa II amesema wao wako tayari kuachia album ila mfumo wa mauzo utakuwa kidijitali zaidi ili kuzuia kazi zao kuibiwa na wasambazaji.

Kala Jeremiah kabadili fleva na muziki??!! Kama vile ambazo tumezoea kumsikia akiwa na midundo ya aina nyingine, sasahivi anarudi na ngoma ambayo anamsifia mwanamke mwanzo mwisho.

Jamaa amesema wimbo huo unampa heshima mwanamke yoyote ambaye anajiona anapendwa na anathaminiwa.

Mkali wa muziki kutoka Zambia, Roberto ambaye kajitambulisha vizuri na mdundo wa AmaRulah ametua TZ kwa ajili ya show kadhaa huku akitupa list ya mastaa wa Bongo TZ ambao tayari amefanya nao collabo.

Roberto amesema tayari ana ngoma na Vanessa na kuna mpango wa kufanya kazi na Shetta na  mastaa wengine pia kama nafasi ikitokea.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments