AyoTV

VIDEO: Mwongozo uliotolewa Bungeni baada ya mauaji ya Askari 8

on

April 18, 2017 mkutano wa saba wa bunge umeendelea ambapo kati ya yaliyojiri ni mwongozo uliotolewa na mbunge wa Bukombe Doto Biteko aliyeomba bunge kuhairishwa ili kujadili tukio la mauaji ya Askari Polisi 8 waliouawa na watu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi yaliyotokea wiki iliyopita.

Ufafanuzi ukatolewa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ambaye alisema…>>>”Kama ilivyotolewa kauli na Waziri Mkuu serikali inalichukulia mambo haya kwa uzito mkubwa na inawahakikishia wananchi

Matukio ya uhalifu yaliyotokea ndio yametupa chachu zaidi ya kupambana na matukio kama haya na pia tunawaomba wananchi watoe taarifa na wala wasiogope maana tuna mfumo bora sana wa kuwalinda watoa taarifa wote” –Waziri Nchemba

VIDEO: “Walitaka kujua nini kitatokea, basi tutawaonesha” – Waziri Mwigulu 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments