AyoTV

VIDEO: Hotuba ya Waziri Nchemba wakati wa kuiaga miili ya askari waliouawa Kibiti

By

on

Usiku wa April 13, 2017 askari polisi wanane waliuawa huku mmoja akijeruhiwa na watu wanaosadikika kuwa majambazi walipokuwa katika doria Wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani.

Leo April 15, 2017 miili ya askari hao imeagwa rasmi katika viwanja vya Polisi Kilwa road ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiongoza viongozi, askari na wananchi kuaga miili hiyo ambapo katika hotuba wakati wa kuiaga miili hiyo aliseema: >>>”Mimi niwaambie tu Watanzania, kitendo kilichofanyika juzi sio cha bahati mbaya, kilipangwa na sisi tutakishughulikia kwa maziringira kama haya. Natanguliza hivi ili Watanzania mutuelewe.

“Wamewashambulia vijana wetu ili waone kitakachofata, sisi tutawaonesha kitakachofuata hatuwezi kuruhusu uhalifu kuendelea na hiki kilichofanyika ni hatua ya mwisho. Wananchi walio wema wajue moja ya ahadi ya serikali ni kulinda usalama wa raia na tutahakikisha tunafanya hilo.” Mwigulu Nchemba.

Nimekuwekea full video bonyeza play hapa chini kutazama…

VIDEO: Ulikosa kutazama tamko la Jeshi la Polisi kuhusu mauaji ya askari wanane yaliyotokea Kibiti? Bonyeza play kutazama.

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo 

Soma na hizi

Tupia Comments