Habari za Mastaa

Kwanini Q Chief alitoa machozi XXL?

on

Kutoka Bongoflevani ukitaja wasanii wakongwe kwenye game sio rahisi kuliacha jina la Shaban Katwila a.k.a Q Chief au Q Chillah kama anavyojiita kwasasa, kupitia XXL ya Clouds FM June 22, 2017 alikuwa On Air kuitambulisha single aliyoshirikishwa na rapa Chid Benz alionekana akiongea kwa hisia kali hadi kutoa machozi.

AyoTV na millardayo.com zimempata Q Chillah Exclusive na ameeleza sababu za yeye kulia wakati akiwa kwenye interview live. Chillah amesema >>> “Niliguswa na hali ya Chid Benz, na najua nimepitia hali nyingi sana kwenye maisha ambazo Chid amepita”

“Lakini kikubwa kilichoniliza nimewahi kuwapoteza marafiki wakubwa sana ambao niliwapenda, wasanii wakubwa, majina makubwa Tanzania mtu kama Albert Mangweha “Ngawair” Mwanahiphop ambaye mimi sijawahi kumuona zaidi yake”<<<  – Q Chillah

Kufahamu zaidi alichokingea Chillah bonyeza play kwenye video hapa chini kutazama.

VIDEO: Unafahamu kwanini Roma hayuko Instagram tena? na mengine ya Magufuli je? Bonyeza play hapa chini kufahamu.

Soma na hizi

Tupia Comments