Top Stories

TCRA yakutana na vyombo vya habari vya mtandaoni

on

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo September 13, 2017 imekutana na vyombo vya habari na kuzungumza kuhusu namna bora ya utoaji taarifa kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni yaani Online Media.

Imesisitiza wamiliki wa vyombo hivyo kuzingatia mambo muhimu yakiwemo uchujaji wa habari, kujali faragha za watu binafsi, matumizi ya lugha na vyanzo na usambazaji wa habari na matukio katika utoaji wa habari hizo.

“Habari za mitandaoni ndizo zinazosambaa haraka zaidi na hivyo ni vyema kukumbushana kuwa uhuru huu wa kutoa habari lazima uendane na wajibu na katika kufuata weledi tunaipa tasnia hii ya habari heshima.” – Valerie Msoka

Ulipitwa na hii? Waziri Kigwangalla leo Bungeni, ni kuhusu wanaume wasiofanya tohara

Hii je? BREAKING: Tamko la haki za binadamu kuhusu hali ya usalama nchini

Soma na hizi

Tupia Comments