Habari za Mastaa

“Nimeishi kwenye mashindano, siku zote naamini kwenye ushindani” – Darassa

on

Rapa staa kutoka Bongoflevani Darassa amesema watu wengi wa Afrika Mashiriki wamekuwa wakiamini kuwa watu wachache tu ndio wanaujua muziki jambo linalotafsiriwa tofauti na wimbo wake wa Muziki.

Darassa ameyasema hayo kwenye XXL ya Clouds FM leo May 4, 2017 akisema kuwa amekuwa akiishi kwenye maisha ya ushindani siku zote na watu wataiona tofauti iliyopo kati ya wimbo wa Muziki na Hasara Roho.

“Kitu ambacho East African wengi wameamini, ndani ya Tanzania kuna watu wachache wanaoweza ila Muziki ulionesha utofauti. Mtu akiamini kwenye kile anachokifanya na kuweka mafanikio, kila kilichokigumu huwa chepesi kwako.

“Nimeishi kwenye mashindano siku zote. Naamini kwenye ushindani, watu wasubiri waone utofauti kutoka Muziki hadi Hasara Roho.” – Darassa

EXCLUSIVE: Ilipofikia video ya Joh Makini na Davido 

Soma na hizi

Tupia Comments