Stori kubwa inayosambaa kwa sasa kutoka Bongomovie ni kuhusu mwigizaji Miriam Jolwa maarufu kama ‘Jini Kabula’ anayedaiwa kutokuwa katika hali ya kawaida ambapo ameomba msaada kwa watu mbalimbali.
Leo August 2, 2017 Ayo Tv na millardayo.com zimemtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba ambaye ameoneshwa kusikitika baada ya kusikia taarifa hizo ingawa hajazipata kwa kina akisema wapo watu watu wamekwenda kumuangalia na watatoa maelezo kwa kina.
Aidha, Mwakifamba amesema taarifa hizo amezipata kupitia mitandao ya kijamii na walikuwa na mpango wa kukutana ili kuangalia namna gani ya kumsaidia.
>>>”Taarifa nimepata kwa juu juu lakini kuna watu ambao wameenda kumuangalia na hao ndio watatupa maelezo kwa kina na baada ya muda kuna sehemu tutakutana tutapata majibu kwa kina. Kwa sasa najua amepata matatizo anaumwa. Ukiangalia unaona kuna tatizo kwenye suala zima la ufahamu wake. Tutajua tatizo linalomkabili nini na msaada gani anahitaji kutoka kwetu.” – Mwakifamba.
Bonyeza Play kumsikiliza zaidi Mwakifamba..
VIDEO: Alichoongea Wema Sepetu leo kwenye kesi yake mahakamani Kisutu