Michezo

FC Barcelona wana siku tano tu za kupatana na PSG kuhusu Neymar

on

Ikiwa bado siku tano kwa dirisha la usajili lifungwe nchini Hispania, uongozi wa FC Barcelona ulikuwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa kwa ajili ya kikao kuhusu Neymar, Barcelona bado wana nia ya kumrejesha mchezaji huyo Nou Camp.

Msafara wa watu wawili wa FC Barcelona akiwemo Eric Abidal walikuwa na kikao kwa muda wa saa nne wakijadili uhamisho huo lakini hawajafikiwa muafaka licha ya Barcelona kutoa ofa ya pound milioni 153 ila bado hawajakubaliana hususani mfumo wa utoaji wao wa pesa..

Barcelona wanataka kulipa pound milioni 153 ili wampate Neymar ila wailipe kwa awamu mbili lakini pia bado wanajishauri kuhusianana uhamisho huo hususani kuridhia Ousmane Dembele aende PSG kama sehemu ya uhamisho wa Neymar kurudi Barcelona kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba 2.

VIDEO: Niyonzima kaeleza kilichotokea kati yake na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments