Michezo

Mahakama imemfungia David Beckham miezi 6 kuendesha gari

on

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England David Beckham amekutana na hukumu baada ya kukutwa na hatia ya kosa lake alilolitenda November 2018, Beckham akiwa na umri wa miaka kwa sasa 44 aliwasili katika Mahakama ya Bromley kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi yake.

David Beckham alikuwa anakabiliwa na kosa la kuendesha gari huku akichezea simu, kosa ambalo alilitenda November 21 2018 akiwa anaendesha gari yake binafsi aina ya Bentley akiwa katika jiji la London, hivyo hilo ni kosa lake la pili analitenda baada ya awali kukutwa na kosa la kuendesha gari kwa spidi.

Kutokana na makosa hayo Beckham amefungiwa miezi 6 kuendesha gari na kupigwa fainai ya pound 750 ambazo ni sawa na Tsh milioni 2.25 huku akitakiwa kulipa pound 100 (Tsh Laki tatu) kama gharama za kuendeshea kesi, pound 35(Tsh laki moja na elfu tano) ya gharama za ziada Beckham amepigwa faini ya jumla ya Tsh Milioni 2.6.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments