Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Kocha Aussems na Bocco wanaendelea kutamba tuzo za TPL

on

Kocha mkuu wa SImba SC Patrick Aussems na mchezaji wake John Raphael Bocco wameonekana kuendelea kutawala katika tuzo za mchezaji bora wa mwezi na kocha bora wa mwezi baada ya kushinda kwa mara ya pili mfululizo.

Bocco ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara 2018/2019 kwa mwezi March, ameshinda tena tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa mwezi April, huku kocha wake mkuu Patrick Aussems aliyekuwa kocha bora wa March nae ameibuka tena mshindi wa tuzo ya  kocha bora wa April.

Tuzo ya mwezi April ilikuwa ikiwaniwa na Heritier Makambo wa Yanga na mchezaji mwenzake wa Simba SC Emmanuel Okwi, huku kocha wake mkuu Patrick Aussems akiwashinda Mwinyi Zahera wa Yanga na Abdul Mingange wa Azam FC, Bocco na Aussems wote wameshinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments