Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limethibitisha kuwa linamshikilia askari wake Kituhu Nashon kwa tuhuma za mauaji ya mtuhumiwa ambaye alikuwa yupo chini ya ulinzi katika kituo cha Kisangara, kamanda wa Polisi mkoa Hamis Issah amethibitisha taarifa hizo.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Hamis Issah ameeleza kuwa tukio hilo lilidaiwa kutokea Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro katika kituo cha Kisangara, anayetuhumiwa kutenda kosa la mauaji kwa kijana Waziri Dhamiri ni askari Kituhu Nashon mwenye namba H 3076.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limepokea taarifa kwa masikitiko makubwa ya kuona mtuhumiwa ambaye alikamatwa na askari wetu wa jeshi la polisi na baadae hali yake ikabadilika na alipopelekwa hospitali mtuhumiwa huyo amefariki, mpaka sasa hivi kilichofanyika askari wa jeshi la polisi tumeshamkamata na yupo chini ya ulinzi”>>>RPC Hamis Issah
“Siwezi kusubiri Rais Magufuli anitumbue mimi”-Naibu Waziri Masauni