Mix

“Hamna ngoma ya Alikiba niliyoitengeneza ikagoma kuwa hit” – Man Water

on

Mashabiki wengi wamekuwa wakijiuliza na wakati mwingine kuacha comments kupitia mitandao ya kijamii kuhusu lini Mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba atatoa wimbo mpya ikiwa ni muda mrefu umepita sasa tangu mwimbaji huyo aachie ngoma yake ya mwisho ‘aje’

Leo July 19, 2017 AyoTV na millardayo.com zimemtafuta Producer Man Water ambaye mara kadhaa amekuwa akifanya kazi na Alikiba >>>”Sasa hivi kuna ujio mwingine wa Alikiba na nimefanya nyimbo zaidi ya nne, yeye ndio atachagua wimbo gani wa kuachia ila makubaliano yetu ni lazima aje kuchukua wimbo wa kuachia, yeye mwenyewe ndio atachagua”

“Huwa tunarekodi nyimbo tunaziweka studio hata kama tumerekodi siku nyingi yeye akija tu anaing’arisha kwa kubadilisha vitu vichache kisha ngoma inakaa sawa zaidi”

“Sijawahi kutengeneza wimbo wa Alikiba ambao haujawa hit hata Mashabiki ni mashahidi kwa mfano tumeona Mwana, Dushelele wengi wakaja wakakopi, hiyo ni mafanikio…Combination mambo yanaenda sawa nashukuru Mungu kila kitu kiko powa.” – Man Water.

VIDEO: Dakika 14 za Alikiba alivyotumbuiza Washington DC…tazama kwa kuplay video hii!!!

FULL VIDEO: Show ya Alikiba Durban South Africa.. itazame hapa chini kwenye hii video

Jionee show ya Alikiba na Ommy Dimpoz Las Vegas Marekani… bonyeza play hapa chini

Tupia Comments