Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Mshtakiwa wa kwanza wa mauaji ya Nipsey akutwa na makosa manne

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Mahakama mjini Los Angeles imemshtaki mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji ya Nipsey Hussle, Eric Holder’29 kwa makosa manne na kuelezwa kuwa kesi yake inawezekana ikawa ina ugumu kumalizika.

Inaripotiwa kuwa Jumanne  ya May 21,2019 mtuhumiwa huyo Eric Holder alisomewa mashtaka hayo ikiwemo moja la kushambulia kwa kutumia silaha, kumiliki silaha kinyume cha sheria ambalo ni kosa la jinai na kuongezewa mashtaka mawili mengine ikiwa ni pamoja na mauaji na kujaribu kufanya mauaji.

Inaelezwa kuwa Eric Holder anatuhumiwa kwa mauaji ya Nipsey Hussle yaliyotokea March 31,2019 na kufanya mashambulio na kuwajeruhi watu wawili nje ya duka la nguo la Marathon Clothing Store.

VIDEO: MOSE IYOBO HAJATOKEA KWENYE BIRTHDAY YA MWANAE, AUNT EZEKIEL KAZUNGUMZA

Soma na hizi

Tupia Comments