Michezo

HALI TETE !!! Haya ndio maisha ya Mourinho na Pogba

on

Moja kati ya video inayosambaa katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni video ya mazoezini ya wachezaji wa Man United, ambapo kwa upande wa Paul Pogba amenaswa na camera akigomewa mkono wake na Jose Mourinho.

Mourinho na Paul Pogba kwa sasa hawako katika maelewano mazuri ila kwa hatua iliyofikia ya Jose Mourinho kugoma kupokea mkono wa salamu wa Pogba, imezidi kuleta tafrani baina ya wawili hao kiasi cha kuanza kutabiriwa kuwa mmoja wao atabidi aondoke.

Inadaiwa kuwa Mourinho ana hasira na Pogba baada ya Pogba kukosoa mbinu za Mourinho baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Wolves, Pogba alinukuliwa na vyombo vya habari kwa kusema kuwa wanahitaji kucheza mfumo wa kushambulia zaidi wakiwa nyumbani na sio mchezo wa kujilinda baada ya kupata goli moja kama wanavyoagizwa.

JB na Ray “Hata Yanga wao wanajua Simba ana timu bora”

Soma na hizi

Tupia Comments