Kamati ya maandalizi ya mbio za riadha za Heart Marathon 2019 safari hii imekutana na waandishi wa habari April 13 ikiwa ni maandalizi na ukaguzi wa njia kwa washiriki wa mbio hizo zitazoanzia Coco Beach April 28 2019, lengo likiwa ni kujenga afya na kuchangia pia matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo.
Mratibu wa mbio za awali za ukaguzi wa njia injinia Patrick Katemba ndio mratibu wa mbio za ukaguzi wa njia “Kwa siku ya leo kwakuwa siku ya April 28 2019 tutakuwa na mbio za Marathon kwa ajili ya uchangiaji wa huduma za matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo, kwa sababu tunaenda kutumia njia mpya inabidi sisi wakimbiaji tujikusanye tufanye mbio ya taratibu ya ukaguzi wa njia kuweza kutambua na kuipita kwa wepesi siku ya mashindano”
Mbio hizo ambazo zitafanyika April 28 zitaanzia Coco Beach na washindi mbali na zawadi ya fedha pia watazawadiwa medali za ushindi wa mbio hizo kama ishara ya kumbukumbu kwa watakaomaliza mbio hizo, mwaka huu utakuwa na maboresho makubwa kama ilivyokuwa kila mwaka kutokana na muitikio wa kuchukua fomu kuwa mkubwa pia.
Mkuu wa masoko wa taasisi ya Tanzania Health Summit Mr Seleman Cheo ambao ndio waandaaji wa mbio za Heart Marathon amezungumzia kukutana kwao na washiriki kabla ya mashindano “Leo tumekutana na wakimbiaji kwa ajili ya kukagua njia itakayotumika katika event yetu ya Heart Marathon, event yetu ipo maalum kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo, event yetu itahusisha mbio za 21KM, 10KM, 5KM na 700KM kwa watoto zote hizo zitakuwa na medali kwa wakaoweza kumaliza”
Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys