Michezo

Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha umuhimu wa Pogba Man United

on

Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Man United yuko mbioni kuihama Man United na kujiunga na Real Madrid ya Hispania kufuatia kuhitajika zaidi na kocha wa sasa wa Real Madrid Zinedine Zidane, leo kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer kaeleza msimamo wake.

Solskjaer kaeleza msimamo wake kuhusiana na tetesi hizo na kutoa kauli ambayo inaivunja Real Madrid nguvu ya kuendelea kumuwinda staa huyo, Ole Gunnar Solskjaer kaeleza kuwa Paul Pogba hawezi kuondoka kwa sasa, kwani ana umuhimu katika kikosi chake, msimamo ambao ni pigo kwa Real Madrid waliokuwa wanaamini kuwa wanaweza kumpata.

Uvumi wa Pogba kuhama ulikuja baada ya Pogba kukiri kuwa Real Madrid ni ndoto ya kila mchezaji kijana“Atatuonesha makubwa hapa kwa sababu nampenda sana kama mchezaji na kama jamaa ni muhimu pia sana kwetu (Man United), hakuna hiyo ishu (kuhama Man United) ni muhimu sana hapa”>>>Ole Gunnar Solskjaer

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments