Michezo

Jezi za timu za LaLiga Hispania kugeuzwa magauni ya watoto kwa upasuaji

on

Moja kati ya habari za kuzipokea leo hii kutokea nchini Hispania, ambapo kampuni ya We Are Xuxa imebuni wazo la kutumika kwa jezi za zamani za timu za Ligi Kuu Hispania LaLiga kwa watoto wanaokwenda kufanyiwa upasuaji, jezi hizo hutengenezwa na kuwa magauni maalumu wanayovaa watoto wakati wakiwa wanafanyiwa upasuaji hospitalini.

Jarida la Soka la Hispania ‘Panenka’ likishirikiana na kampuni ya ‘We Are Xuxa’ wameanza kuzibadilisha jezi (fulana) za zamani za timu za La Liga na kuwa magauni ya kuvaa Watoto wakati wakifanyiwa operesheni hospitalini ili kuwasaidia Watoto hao kupona haraka.

Sababu kubwa ya kufikiria wazo hilo ni kutokana na kuaminika kuwa upasuaji ni jambo la hatari na wakati mwingine linaweza kugharimu maisha, sasa kuwavalisha watoto jezi hizo za timu wanazozipenda ni kuwaandaa kisaikolojia kuwa wanaenda kucheza mechi (upasuaji) ngumu ambayo wanapaswa kupambana na kushinda.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments