Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

EXCLUSIVE: Kocha wa Simba SC kazungumzia hatma ya Okwi na Niyonzima

on

Moja kati ya habari zinazochukua headlines kwa sasa Tanzania katika soka la bongo ni habari za usajili wa wachezaji ambapo Yanga SC tayari wameanza usajili huo vipi kwa upande wa watani zao Simba SC?
.
AyoTV imefanya Exclusive Interview na kocha Mkuu wa Simba SC Patrick Aussems na kumuuliza kuhusiana na mipango yake vipi kuhusiana na usajili? vipi kuhusiana na Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima wanaomaliza mikataba yao wanabaki au wanaondoka SImba? maana Okwi hata kwenye usiku wa tuzo hatujamuona?
.
“Hatutahitaji mchezaji wa katika kila nafasi lakini tunahitaji beki, kiungo na mshambuliaji kama tunataka kwenda mbele zaidi katika michuano ya Afrika tunahitaji kuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu na wiki ijayo mtawajua wachezaji wa Simba, Emmanuel (Okwi) anamaliza mkataba wake tutajua nini kinaendelea kama ataamua kwenda kwenye klabu nyingine tutalazimika kutafuta mbadala wake”>>>Aussems
.
“Kuhusu Haruna ni sawa na Okwi tuna wachezaji wanne au watano ambao wanamaliza mikataba yao na Simba bodi na uongozi unazungumza nao tutaona kama tutafikia makubaliano nao kama hatutofikia makubaliano nao tutatafuta wachezaji wengine rahisi tu”>>>Aussems


EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments