Michezo

Waziri Mkuu wa Bulgaria kashindwa kuvumilia ubaguzi waliofanyiwa wachezaji wa England

on

Waziri mkuu wa Bulgaria  Boyko Borissov ameoneshwa kukerwa kwa kitendo cha mashabiki wa soka wa Bulgaria kuwafanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi wachezaji wa England wakati wa mchezo dhidi ya timu hizo mbili zilipokutana nchini Bulgaria katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Euro 2020.

Boyko Borissov amemshinikiza Rais wa shirikisho la soka nchini Bulgaria Borislav Mihaylov ajiuzulu nafasi yake hiyo kwa kuamini kuwa kuna uzembe ulifanyika hadi vitendo hivyo vya ubaguzi vikafanyika uwanjani, tena na mashabiki ambao wanaonekana walijiandaa mapema na mabango ya kuwabagua England.

Waziri mkuu wa Bulgaria Boyko Borissov

Mashabiki wa Bulgaria katika mchezo huo walioshuhudia timu yao ya taifa ikipoteza 6-0 dhidi ya England, waliingia na hood, t shirt na mabango yanayoonesha kuwa walidhamiria kufanya kitendo hicho, licha ya kabla na wakati wa mchezo kutolewa tangazo kuwa vikitokea vitendo vya kibaguzi muamuzi atavunja mchezo mashabiki wa Bulgaria hawakukoma.

Kushoto ni Rais wa shirikisho la soka Bulgaria Borislav Mihaylov

VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA

Soma na hizi

Tupia Comments