Michezo

Vincent Kompany kainusuru Man City, Leicester City nusura waharibu shughuli

on

Club ya Man City ya England ambayo inapambania kwa sasa kutetea taji lake la Ligi Kuu ya England msimu wa 2018/2019, hivyo walicheza game yao muhimu na mwisho nyumbani dhidi ya Leicester City game ambayo ni muhimu kwa kupata matokeo ili kujiweka nafasi nzuri ya kutetea taji lao la Ligi Kuu England.

Man City wakiwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 goli ambalo lilifungwa na nahodha wao Vincent Kompany dakika ya 70 akiwa nje ya 18 kwa shuti kali, hiyo ni baada ya ukuta wa Leicester City kuwa imara na kushindwa kupenyeka kirahisi kiasi cha kujikuta wakicheza dakika 69 bila kupata goli lolote, Leicester kama wangetoka sare leo wangewaharibia Man City ambao wameanza kusherehekea kimya kimya taji la EPL.

Ushindi huo unawarudisha Man City kilele mwa msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa wamecheza michezo 37 sawa na Liverpool na wakiongoza kwa point 95 wakifuatiwa na Liverpool wenye point 94, wote wamesalia na mchezo mmoja kumaliza Ligi Man City atakuwa ugenini dhidi ya Brighton na Liverpool atakuwa nyumbani dhidi ya Wolves huku akiiombea mabaya Man City wateleze ili watwae taji la EPL kwa mara ya kwanza baada ya miaka 29.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments