Michezo

PSG imetangaza Neymar atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne, hizi ndio mechi atazikosa

on

Kufuatia kuumia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar, kumeonekana kuwa na madhara zaidi baada ya club yake ya PSG kutangza kuwa mchezaji huyo ameumia na atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne sawa na mwezi mmoja.

Neymar atakuwa nje ya uwanja  kutokana na kuumia nyama za paja, jeraha ambalo alilipata wakati akiichezea timu yake ya Taifa ya Brazil katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria uliyomalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 mchezo huo ukichezwa nchini Singapore.

Katika mchezo huo Neymar alicheza kwa dakika 12 tu na kushindwa kuendelea na mchezo, ila PSG imetoa taarifa kuwa Neymar baada ya kupimwa katika kipimo cha MRI anaumwa nyama za paja za mguu wa kushoto, Neymar sasa atakuwa nje ya Uwanja hadi November 11 akikosa michezo minne ya Ligue 1 ukiwemo dhidi ya Marseille October 27 na michezo miwili ya nyumbani na ugenini ya UEFA Champions League dhidi ya Club Bruge

VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA

Soma na hizi

Tupia Comments