Habari za Mastaa

Duh! Nelly asimamisha show kisa shabiki kafungua kamba za viatu vyake (+Video)

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa staa wa muziki wa Rap Nelly aliamua kugeuza kibao kwa mashabiki zake na kuikatisha show kwa muda mchache baada ya shabiki kutaka kujaribu kumfungua kamba za viatu vyake alipokuwa akipanda stejini kwa ajili ya kutoa burudani.

Kwa mujibu wa video iliyopostiwa na mtandao huo Nelly alisikika akisema “Babygirl, naukubali upendo wako lakini kwanini unifungue viatu? Hapana hapana, huwezi kunifungua viatu, kama unataka kunitega sasa hilo ni jambo lingine, Imenilazimu kusimamisha na kufunga upya”.

Nelly alizidi kusisitiza kuwa haihitaji mtu kumfungua kamba za viatu vyake ikiwa tayari ni mtu mzima na mashabiki hawahitaji kuwa na uhuru wa kiasi hicho alisema hayo kwenye show yake mjini Las Vegas Marekani kwenye moja ya kumbi za starehe za Drai’s Beach club.

VIDEO: ULIPITWA NA MAJIBU YA PIERE JUU YA PICHA YA KIMAHABA NA AMBER LULU, NI WAPENZI..? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments