Habari za Mastaa

Roma Mkatoliki “Ukitualika tunakuja tunafuturu tunapiga selfie tunasepa”

on

Kama umefuatilia hivi karibuni Wasanii mbalimbali wamejitoa kufuturisha watu kadhaa katika jamii ikiwa ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo kumekuwa na comments nyingi kuhusiana na hicho ambacho wasanii wamekua wakikifanya.

Msanii kutokea kwenye industry ya muziki wa Hip Hop Roma Mkatoliki ametoa mawazo yake kuhusu hilo huku akisema kuwa wengi wanaoalikwa wanakuwa hawajafunga na wengi hufanya hivyo sababu wanajua kuwa wasanii hao wanafollowers kwa hiyo wakipost kupitia kurasa zao basi wataonekana kinachotakiwa ni kualika watu wenye uhitaji watashukuru na kuomba dua.

Msanii Rama Dee ameonekana kujibu kile ambacho Roma amekiandika kupitia ukurasa wake wa twitter na yeye akaamua kuandika mawazo yake kuhusiana na kauli hiyo na kusema kuwa “Ukiona mwalika futari amekosea kualika watu andaa yako alafu alika watu wako au andika wimbo wa Rap wivu sema ile futari haikuwa tamu ni ftari ya selfie”

VIDEO: KUTOKA SUMBAWANGA, MASHABIKI WALIVYOJIANDAA KUIPOKEA NANDY FESTIVAL

Soma na hizi

Tupia Comments