Habari za Mastaa

Alikiba “Sitoagi ngoma siku ya Jumanne”

on

Leo October 8,2018 Alikiba pamoja na wasanii wa record label yake ya Kings Music wametambulisha rasmi ngoma yao ya ‘Mwambie Sina’ katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm pamoja na kufanya mahojiano.

Alikiba amezungumza vitu vingi kuhusiana na record label hiyo pamoja na ngoma yake ya Hela ambayo iliachiwa na baadae kufutwa kwenye mtandao wa You Tube.

“Nimeamua kuwachukua vijana hawa kwanza kwasababu wana vipaji halisi, wamefuzu vigezo vyote vya muziki. Nimekuwa kwa miaka miwili nikiwapika sasa hivi wapo tayari kuingia kwenye industry rasmi”

“Kikubwa kilichonivutia kwa vijana hawa wapya ni kipaji, nimewapa training kiasi na waliponiridhisha nikaamua kuwaleta kwenu nyinyi”

“Nilishawahi kuwa label lakini haikuwa rasmi, wazo hili lilinijia wakati nipo G-Records, niliona mimi nilivyosaidiwa, nikasema na mimi Allah akinijaalia uwezo nitasaidia vijana wengine.”

“Lengo langu ilikuwa kutoa hela kwenye siku ya arobaini ya dancer wangu aliyefariki na nilifanya hivyo ili kumuenzi kwasababu alitunga style zote za kwenye wimbo huo nilitaka dancers wote wawepo na wacheze”

“Hela ilitolewa kimakosa na mtu ambaye anahusika na You Tube na akaitoa siku ya Jumanne siku ambayo huwa sitoi nyimbo, kwahiyo wimbo huo haukuwa rasmi kama wangu kwasababu nilikua na ngoma rasmi ambayo ni mwambie sina”

BREAKING: Watumishi 11 wa benki wanaswa na TAKUKURU

Soma na hizi

Tupia Comments