Habari za Mastaa

Hamisa Mobetto kuachia ngoma ya nne na Christian Bella

on

Mwimbaji na muigizaji Hamisa Mobetto ametuonyesha kuwa yupo mbioni kuileta kazi yake mpya akiwa pamoja na mkali wa muziki wa dansi Christian Bella hii ni baada ya wawili hao kuonekana wakiwa Falme za Kiarabu Dubai.

Picha nyingi pamoja na videos zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha wawili hao wakiwa kwenye kazi, hii ni baada ya maneno mengi kusambaa ambapo baadhi ya watu wamekua wakidai kuwa huenda Hamisa akawa yupo Dubai na mwanaume mwingine ambaye ana uwezo kifedha kwa jailli ya kula bata.

Kumbuka kuwa hii itakuwa ni kazi ya nne ka Hamisa kuachiwa rasmi ambapo kazi yake ya kwanza ilikua Madam Hero aliyoiachia Sept 18,2018 ya pili Tunaendana na akamalizia na ngoma ya My Love.

“Sheri nalingaka yo mingi yo ozali mobali ya vie na ngai ata balobi se pamba nga nakolinga kaka yo je t’aime je t’aimerais pour toujours motema na ngai 🎶🎶#BOSS Loading @bellachristian1 X @hamisamobetto🔥🔥” aliandika Hamisa Mobetto kupitia ukurasa wa instagram

VIDEO: WANANCHI WAMUOMBA DC WAMUUE MBAKAJI “NINA CHUNGU SANA TUUE”

Soma na hizi

Tupia Comments