Habari za Mastaa

Pierre Likwidi amemkabidhi DC Jokate madawati 20 (+picha 8)

on

Fahamu kuwa Pierre Ghumbo maarufu kama ‘Mzee wa Likwidi’ amekamilisha ahadi aliyoitoa kwa DC wa Kisarawe Jokate Mwengelo siku ya Harambee ya ‘Tokomeza Zero’ iliyofanyika March 30,2019 ambapo leo May 21,2019 amekabidhi jumla ya madawati 20 kwaajili ya kuwasaidia wanafaunzi.

DC Jokate Mwegelo amemshukuru Pierre kwa kukamilisha ahadi yake na kutoa madawati ambayo yamezidi thamani ya pesa mabyo aliitaja kuitoa ambayo ilikua laki moja, kupitia ukurasa wa instagram wa Jokate ametoa shukrani hizo akiwajumuisha na wananchi wa Kisarawe.

“Ahadi Imetimia!!! Leo nimepokea madawati 20 yenye viwango vya juu kutoka kwa Pierre Liquidi chini ya kampuni ya Afro Furnishers and Hardware. Kwenye Harambee yetu ya tarehe 30/03/2019 aliahidi kutoa laki moja lakini leo amekuja na madawati 20 yenye thamani ya zaidi ya tsh laki moja aliyoahidi. Kwa niaba ya Wanakisarawe nasema asante sana kwa mchango wako bado ahadi ya kutengeneza madawati na hii kampuni inabaki. Asante” >>> Jokate Mwegelo 

VIDEO : NANDY AONYESHA STUDIO YAKE ALIYOJENGA NYUMBANI, KAONGELEA SHOW YA SUMBAWANGA NA MTOTO WA RUGE

Soma na hizi

Tupia Comments