Ad

Michezo

Yalivyokuwa mazishi ya Diego Maradona (+picha)

on

Vyanzo mbalimbali vya habari nchini Argentina vimeripoti kuwa Diego Maradona amezikwa mapema na watu wachache ambao ni wanafamilia na rafiki wa karibu sana na Maradona kwenye makaburi ya Ardin Bella Vista pembeni ya walipozikwa wazazi wake Dalma na Diego.

Mazishi ya gwiji huyo yameongozwa na rais wa nchi hiyo Alberto Fernandez akiwa amevaa jezi ya Argentinos junior ambayo ndiyo timu ya kwanza Maradona kuanza kuichezea, huku mke wa Rais huyo Fabiola Yañez akiwa amevaa vazi la maua wakati wa maziko hayo.

Mamia waliojitokeza kutaka kuhudhuria mazishi hayo hawakuruhusiwa na vyombo vya usalama kutokana na kinachodhaniwa kuwa Maradona huenda alifariki kwa ugonjwa wa Corona hivyo wamefanya jitihada za kukwepa mkusanyiko wa makusudi kujihadhari na ugonjwa huo.

Licha ya mamia hao kuishia kutoa heshima zao za mwisho jana jioni, leo wameendelea kujitokeza kwenye mitaa wakiimba wimbo wa taifa wakiwa wamevaa jezi za maradona kuelekea  Gaza de mayo eneo ambalo walifurahi pamoja na maradona baada ya kubeba kombe la dunia 1986.

MDEE NA WENZAKE WAVULIWA UANACHAMA CHADEMA “WASIJIHUSISHE KWA NAMNA YOYOTE ILE” FREEMAN MBOWE

Soma na hizi

Tupia Comments