Habari za Mastaa

Ile ndoto ya Mtoto wa TMK imetimia, Said Fella azungumzia show ya Yamoto band London

on

.

.

Imagine Ndoto ya mtoto wa TMK ambaye aliwahi kusema hajutii kutokea kwenye familia ya kimasikini leo ndoto yake ya kutembelea nchi mbalimbali duniani imetia, anatembelea hizo nchi na analipwa.

Niliwahi kuzungumza na Asley akaniambia kuna mengi bado hajayatimiza kwenye maisha yake japokuwa kwa kiasi chake anaona mabadiliko toka ameanza kufanya muziki, ni mtoto ambaye ametoka kwenye familia isiyo na uwezo wa kifedha.

Kuna siku niliwahi kwenda nyumbani  kwa wazazi wake mwendo wa dakika  kama 60 nje ya mji  wa Dar es Salaam, wazazi wake walifurahi sana na  wakanichukua mguu kwa mguu mpaka kwenye nyumba ambayo wakati huo Asley alikuwa anawapa pesa  kidogo kidogo waijenge, nilipokwenda kuiona ilikuwa imefikia kwenye rent.

.

Pichani:Asley akiwa kwenye ndege kuelekea nchini Uingereza kwenye show yao.

Kama ulikuwa hajui pia  muimbaji huyo kiongozi wa Yamoto Band, Asley aliwahi kukasirishwa sana  na kuumia moyoni kwa muda mrefu  kwa kisa cha Baba yake mzazi kufungwa polisi baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba ambayo walikuwa wakiishi na ndio maana akajipanga mpaka kuwasaidia wazazi wake na kumpa mama yake mzazi pesa ya mtaji.

Leo hii Asley anaendelea kupokea baraka za wazazi milango inafunguka na sasa yeye na Yamoto Band wameondoka Tanzania kwenya Uingereza.

.

Pichani Yamoto Band wakiwa wameshawasili nchini Uingereza.

Akiongea kwenye Amplifaya ya Clouds FM alisema: ‘Hii ni mara yetu ya kwanza kwa Yamoto Band ndio tunaenda , tunamshuru mwenyezi Mungu kwa hiyo itakuwa ni safari yetu ya kwanza huko tutakaa wiki mbili, tuna show mbili lakini bado show moja hatuja confirm, show ya kwanza itakuwa tarehe 21 na show ya pili itakuwa tarehe 22, kusema kweli tuna vitu vingi vya kuzungumza unajua wengine ndio mara yetu ya kwanza kwa hiyo vitu vingi tunakuwa na hamu navyo kama barabara zao, magorofa na vitu vingi tu, asilimia 90 za sehemu tulizofanya show yaani show zetu watu wanakubali vizuri lakini Arusha wanatuonesha maajabu sana kwasababu sisi tunaamini  kule ni  Hip Hop halafu ukiingia kwenye show unakuta watu wamejaa”–alisema.

.

.

Naye mkurugenzi wa taasisi ya Mkubwa na Wanae,  Yamoto Band na Wanaume Family Said Fella akazungumza machache kuhusiana na show ya Yamoto Band nchini Uingereza na kusema ;…‘Niliwauliza tu kwasababu siwezi kushangaa maana TMK wameshawahi kwenda na pia hata Naseeb, kwa hiyo niliwauliza kwa Yamoto Band wanataka kwa CD au Live wakaniambia kuwa wanataka muziki wa Live nikasema muziki tulioubuni ndio huo sasa unatambulika sasa duniani, mpaka sasa mkataba wetu tuliofanya na kampuni ya Zuri kwamba tumekubaliana yamoto watakuwa na  show mbili London’–alisema.

Unaweza uka bonyeza play kusikiliza interview hiyo.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments