Michezo

“Yanahitajika mabadiliko makubwa ndani ya Barcelona” Pique

on

Beki wa Klabu ya Barcelona, Gerlad Pique amesema kikosi chao kinahitaji mabadiliko makubwa kama wanahitaji kurejesha ubora wao.

Kauli hiyo inafuatia Barcelona kutandikwa vilivyo na Bayern Munich kwa jumla ya mabao 8-2 katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya uliopigwa usiku wa jana.

Raia huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 33, amesema hata yeye yupo tayari  kuwa mchezaji wa kwanza kuondoka kuruhusu mabadiliko hayo iwapo Klabu itabariki.

Pique ambaye katika miaka yake 12 akiwa na Barcelona ameshinda mataji 20, ameongeza kuwa wanapaswa kuwajibika akianza Kocha na kisha wachezaji wafuatie.

BONDIA HASSAN MWAKINYO ALIVYOMPIGA TSHIBANGU WA CONGO NA KUWA BINGWA WA WBF

Soma na hizi

Tupia Comments