Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amekosoa vikali kuhusika kwa nchi za Magharibi nchini Afghanistan kama jaribio la kulazimisha demokrasia nchini humo.
Papa amezungumzia suala hilo kwa kutumia maneno ya Rais wa Urusi Vladimir Putin akifikiria kwamba anamnukuu Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Alipoulizwa swali kuhusiana na Afghanistan katika mahojiano na kituo kimoja cha redio mjini Marid, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amesema atajibu kwa nukuu ya Kansela wa Ujerumani ambaye anamchukulia kama mmoja wa wanasiasa wakuu duniani ingawa maneno aliyoyasema yalisemwa na Rais Putin mwezi uliopita mjini Moscow alipotembelewa na Kansela Merkel.
Papa amesema ni makosa iwapo mtu atashurutisha wengine kufuata yale anayoyataka yeye bila kuzingatia tamaduni na dini yao.