Michezo

Yanga SC watest mitambo kwa Mlandege FC

on

Club ya Yanga SC leo imecheza mchezo wake wa kirafiki kuelekea mechi yake ya Ligi Kuu Tanzania bara itakayochezwa weekend hii Bukoba dhidi ya Kagera Sugar.

Kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu leo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege FC ya Zanzibar katika uwanja wa Chamazi jijini Dar Es Salaam na kupata ushindi wa magoli 2-0.

Magoli ya Yanga ambao leo waliwatumia jumla ya wachezaji wake 22, yalifungwa na Waziri Junior kwa penati dakika ya 40 na Tonombe Mukoko dakika ya 59 baada ya kupokea pasi safi ya Sarpong.

Yanga SC haikupata mechi za kirafiki ukizingatia kocha Zlatko Krmpotic aliyejiunga na Yanga siku chache kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania bara.

Soma na hizi

Tupia Comments